Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania yaiuzia Zambia mahindi tani 650,000

Mahindi Tanzania yaiuzia Zambia mahindi tani 650,000

Mon, 1 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kutokana na ukame unaoikumba nchi ya Zambia, nchi hiyo imeingia makubaliano na Tanzania kununua tani 650,000 za mahindi kwa ajili ya kuwasaidia wananchi milioni saba wa taifa hilo.

Mkataba huo utatekelezwa kwa kipindi cha miezi nane na utaiingizia Tanzania dola milioni 250 sawa na Sh650 bilioni.

Mahindi hayo yatakayosafirishwa kwenda Zambia yatatolewa katika maghala ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) ambapo kwa kituo cha Songwe mahindi tani 55,000, Makambako tani 75,000, Sumbawanga tani 250,000 na Songea tani 270,000.

Mkataba huo umesainiwa na Mkurugenzi Mkuu wa NFRA, Dk Andrew Komba pamoja na Mratibu wa Maafa kitaifa nchini Zambia Dk Gabriel Pollen, wakishuhudiwa na Waziri wa Kilimo Hussein Bashe, Waziri wa Fedha Dk Mwigulu Nchemba na Waziri wa Kilimo Zambia Reuben Phiri.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live