Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania yaitumia kimakati mkutano wa Uganda

January Makamba Kuongoza Usalama Bomba La Mafuta Tanzania yaitumia kimakati mkutano wa Uganda

Fri, 19 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Takribani theluthi mbili ya nchi duniani zimekusanyika jijini Kampala, Uganda kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Nchi Zisizofungamana na Upande Wowote (NAM) wenye nchi Wanachama 120 na Mkutano wa nchi za Kundi la 77 na China (G77+China) lenye Wanachama 134.

Tanzania ni mwanachama hai wa jumuiya hizo, hivyo inashiriki kikamilifu katika ngazi zote za mikutano hiyo iliyoanza tarehe 15 Januari na itahitimishwa tarehe 22 Januari 2024.

Kwa ngazi ya mawaziri, January Makamba, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, ameongoza ujumbe wa Tanzania katika mkutano wa siku mbili wa ngazi ya mawaziri uliokamilika jana tarehe 18 Januari 2024.

Pembezoni mwa Mkutano huo, Makamba alikutana na mawaziri wenzake kwa lengo sio tu la kukuza na kuimarisha ushirikiano wa kidiplomasia na nchi marafiki, bali pia kuweka mikakati ya kushirikiana kiuchumi na kuondoa changamoto zinazokwamisha jitihada za kukuza uchumi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live