Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania yaingia mkataba wa kununua Airbus mbili

76441 Atcl+pc

Thu, 19 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Wakala wa Serikali na kampuni ya utengenezaji wa ndege ya Airbus wamesaini mkataba wa ununuaji wa ndege mbili aina ya Airbus A220-300 ambazo zitatumiwa na Shirika la ndege la Tanzania (ATCL).

Mkataba huo umesainiwa leo Alhamisi Septemba 19, 2019 Airbus imewakilishwa na Makamu wa rais wa kampuni hiyo Afrika, Hadi Akoum na upande wa Serikali alikuwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa wakala wa Ndege za Serikali, Benjamin Ndimila.

Akizungumza mara baada ya kusaini mkataba huo, Ndimila ambaye hakutaja gharama halisi inayotumika kununua ndege hizo amesema ndege hizo zitakuwa na tofauti na za aina hiyo ambayo tayari zinatumiwa na ATCL kwani kila kiti kitakuwa na 'skrini' "jambo hii ni historia inaacha historia".

Kwa upande wake, Akoum amesema uchongaji wa ndege ya aina hiyo unachukua mwaka mmoja hadi mwaka mmoja na nusu na kwa sasa kuna oda nyingi lakini ndani ya kipindi hicho anatumaini itakuwa imekamilisha.

"Uchongaji wa ndege sio jambo rahisi linachukua muda na kwa ndege za aina hii kwa kawaida huchukua mwaka mmoja hadi mwaka mmoja na nusu na sasa tuna oda nyingi tunapaswa kuzalisha ndege walau mbili na nusu za aina hiyo kwa siku ili kwenda na oda zilizopo," amesema Akoum.

Chanzo: mwananchi.co.tz