Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania yadaiwa kuilipa Sh75 bilioni kampuni ya Winshear

Pesa Fedhaddd Tanzania yadaiwa kuilipa Sh75 bilioni kampuni ya Winshear

Tue, 17 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kampuni ya madini ya Winshear Gold katika tovuti yake imedai kumaliza mgogoro baina yake na Serikali ya Tanzania kwa kulipwa Sh75 bilioni Kama stahiki yao.

Katika taarifa hiyo ambayo pia imechapishwa katika mitandao mbalimbali ya kimataifa ikiwamo, Financial post imesema kuwa fedha hizo zimelipwa leo Jumatatu Oktoba 16, 2023 na Serikali ya Tanzania.

Hata hivyo, Septemba 22, 2023 akizungumza na gazeti dada la The Citizen Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dk Eliezer Felesh alikiri kuwapo kwa kesi hiyo huku akisema timu za usuluhishi zinaendelea na mazungumzo chini ya usimamizi wa Kituo Cha Kimataifa Cha Usuluhishi wa Migogoro ya Uwekezaji.

Hatua hiyo inakuja baada ya Kampuni ya Winshear gold kuishtaki Tanzania kutokana na uamuzi wa kufuta leseni za kampuni hiyo iliyokuwa ikiendesha mradi wa dhahabu wa SMP, uliopo Kusini Magharibi mwa Tanzania.

Leseni za Winshear zilifutwa mara tu baada ya Serikali kurekebisha Sheria ya Madini ya 2010, ambayo kanuni zake zilifuta leseni zote za uhifadhi, na wakati huo zilikoma kuwa na athari yoyote ya kisheria.

Richard Williams, Mkurugenzi Mtendaji wa Winshear Gold, alieleza mwafaka huo kuwa mzuri kwa Tanzania na Winshear, na kubainisha kuwa amefurahishwa na kufikia hitimisho lililokubalika na pande zote mbili.

"Ni wakati wa pande zote mbili kuendelea, na tunaitakia Tanzania mafanikio katika kuvutia uwekezaji mpya.

"Kampuni inashukuru kwa dhati timu yetu ya wanasheria kwa kazi yao ya kuandaa na kuwasilisha kesi yetu,” alisema Williams.

Usikilizaji wa ushahidi kati ya kampuni hiyo na Serikali ya Tanzania ulianza Februari 13, 2023, mjini Washington ambapo jopo la watu watatu lilisimamia vikao vya Mahakama vilivyotarajiwa kukamilika kabla ya kufungwa kwa shughuli hiyo Ijumaa Februari 17, 2023.

Serikali iliondoa umiliki wa Winshear katika mradi wa SMP jambo ambalo ilisema kufanya hivyo, Tanzania ilikiuka wajibu wake kwa Winshear chini ya mkataba wa uwekezaji wa nchi baina ya Canada na Tanzania (BIT) na sheria za kimataifa.

Baadhi ya hayo ni pamoja na wajibu wa Tanzania wa kutotaifisha au kunyang'anya vitega uchumi vya kampuni au kuwekewa hatua zinazolingana na kutaifishwa au kunyang'anywa mali bila fidia ya haraka ya kutosha na yenye ufanisi chini ya BIT.

Mkataba wa Kituo cha Kimataifa cha Usuluhishi wa Migogoro ya Uwekezaji (ICSID) umeridhiwa na Mataifa 158, Tanzania ikiwamo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live