Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania yaanza uchorongaji madini ya Helium

MAVUNDEEEEEE Tanzania yaanza uchorongaji madini ya Helium

Fri, 27 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Madini, Anthony Mavunde amebainisha kuwa leo Tanzania imeweka historia ya kuanza uchorongaji madini ya Helium ambapo huko mkoani Rukwa kampuni ya Noble Helium imepeleka chini regi yao kwa mara ya kwanza hivyo kuandika historia hiyo.

Akizungumza na wadau wa sekta ya madini katika jukwaa la uwekezaji sekta ya madini Tanzania lililofanyika mkoani Dar es Salaam, Mavunde amesema kuwa kwa Tanzania ni historia kubwa na itakuwa ni kazi kubwa ya kwanza katika historia ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kufanyika kwenye sekta ya madini.

“Tanzania tunaandika na sisi historia leo tarehe 26 kuanza kazi hii ya uchorongaji pale mkoani Rukwa tukiamini kwamba itatoa mchango mkubwa kwa ustawi wa taifa letu la Tanzania kupitia sekta ya madini,” amesema Mavunde.

Ameongeza kuwa madini hayo yana umuhimu mkubwa ambapo hutumika katika shughuli mbalimbali ikiwemo utengenezaji wa vifaa vya simu na kompyuta pamoja na vile vya matibabu kama vile ‘MRI’.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live