Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania ya viwanda yavutia wawekezaji wa nje

Thu, 22 Nov 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kampuni ya Emerson inayotengeneza mitambo na vipuri  duniani imetoa mafunzo bure yatakayosaidia wadau kutoka taasisi mbalimbali, kuongeza ujuzi katika mashine za kupima viwango na ubora wa mafuta na gesi nchini maarufu flow meters.

Kampuni hiyo kwa kushirikiana na kampuni ya Petrogas wametoa mafunzo hayo leo Novemba 21, 2018 jijini Dar es Salaam kwa washiriki 52 waliowakilisha kampuni binafsi na umma nchini. 

Mafunzo hayo yamejikita katika mita mbili zinazotengenezwa na kampuni ya Emerson, ambazo ni Micro Motion Coriolis Flow Meters  zenye umbo la herufi U na Daniel Ultra Sonic Flow Meters.

Kiongozi wa jopo la watalaamu wa kampuni ya Emerson kutoka nchini Marekani, William Fernandes amesema faida za mafunzo hayo ya siku moja kwa Tanzania iliyojikita kwenye uchumi wa viwanda, yataongeza uwezo wa kutambua ubora wa bidhaa hizo katika masoko ya nje.

Hata hivyo, Fernandes amesema tayari kuna mitambo ya kampuni mbalimbali nchini za gesi na mafuta zilizofunga mita hizo na kuonyesha mafanikio makubwa.

Amezitaja kampuni zilizofunga mita hizo ni Shirika la Taifa la Maendeleo ya Petroli (TPDC), Pan African Energy Tanzania (PAET), Maurel na Prom.

Mwakilishi wa Petrogas, Greyson Kiondo amesema Emerson baada ya mafunzo hayo yanayotolewa kwa vitendo, washiriki watakuwa pia na maarifa ya kutosha katika mitambo mbalimbali ikiwamo mita za kupima kiwango cha vimiminika.

Mbali na hilo, Kiondo amesema hatua hiyo itasaidia pia kutambua gesi za aina zote ikiwamo mafuta wakati wa kufanya biashara.

 

 



Chanzo: mwananchi.co.tz