Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania ya tatu mazingira mazuri ya uwekezaji Afrika

Kitila Tanzania ya tatu mazingira mazuri ya uwekezaji Afrika

Tue, 31 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo amesema kulingana na tafiti za Kimataifa, Tanzania ni nchi ya tatu kwa mazingira mazuri ya Uwekezaji Barani Afrika ikitanguliwa na Nigeria na Afrika Kusini.

Profesa Mkumbo amesema hayo mkoani Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa Jukwaa la Biashara lililowakutanisha wawekezaji kutoka Tanzania na Ujerumani.

Amesema maeneo waliyojadiliana ambayo Ujerumani inaweza kuwekeza ni pamoja na nishati jadidifu, kuzalisha umeme wa maji, jua na upepo na pia uzalishaji wa madini ya kimkakati ya kutengeneza betri na kuunganisha magari ikiwemo Volkswagen.

Jukwaa hilo la Biashara lililowakutanisha wawekezaji kutoka Tanzania na Ujerumani pia limejumuisha viongozi wa Serikali pamoja na wawekezaji mbalimbali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live