Matumizi ya internet yameonekana kuongezeka kwa kasi na bara la Afrika lenye Nchi 54 ni moja kati ya Mabara yanayotarajiwa kuona ukuaji mkubwa wa kiuchumi kutokana na teknolojia.
Tanzania imeshika nafasi ya 10 katika orodha ya nchi zenye idadi kubwa za Watumiaji wa intaneti Afrika kwa mwaka 2022 kwa mujibu wa DataReportal.
1. Nigeria - Kulikuwa na Watumiaji milioni 109.2 wa intaneti nchini Nigeria mpaka Januari 2022.
2. Misri - Watumiaji milioni 75.66 wa intaneti nchini Misri mpaka Januari 2022.
3. South Africa - Watumiaji milioni 41.19 wa intaneti nchini Afrika Kusini mpaka Januari 2022.
4. Morocco - Watumiaji milioni 31.59 wa intaneti nchini Morocco mpaka Januari 2022.
5. Ethiopia - Watumiaji milioni 29.83 wa intaneti nchini Ethiopia mpaka Januari 2022.
6. Algeria ——— Watumiaji milioni 27.28 wa intaneti nchini Algeria mpaka Januari 2022.
7. Kenya ——— Watumiaji milioni 23.35 wa intaneti nchini Kenya mnamo Januari 2022.
8. Ghana ——— Watumiaji milioni 16.99 wa intaneti nchini Ghana mpaka Januari 2022.
9. DR Congo ——— Watumiaji milioni 16.50 wa intaneti nchini DRC mpaka Januari 2022.
10. Tanzania ——— Watumiaji milioni 15.60 wa intaneti nchini Tanzania mpaka Januari 2022.