Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania na Uganda zasaini mikataba ya sekta ya mafuta na gesi

117963920 Museveni2 Tanzania na Uganda zasaini mikataba ya sekta ya mafuta na gesi

Mon, 12 Apr 2021 Chanzo: mtanzania.co.tz

Kampala, Uganda

Tanzania na Uganda zimesaini mikataba katika maeneo matatu muhimu ya kuendeleza sekta ya mafuta na gesi ya Uganda.

Mikataba hiyo imesainiwa jana Aprili 11, 2021 wakati wa ziara ya kwanza ya nje ya nchi ya Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

Utiaji saini huo umefanyika kati ya Serikali ya Uganda na Kampuni ya Mafuta ghafi ya Afrika Mashariki (EACOP) juu ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima (Uganda) kwenda Tanga (Tanzania).

Makubaliano kati ya mataifa hayo mawili ya Afrika Mashariki yamejikita katika masuala ya hisa, usafirishaji na ushuru.

Mradi huu una manufaa makubwa kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki, ni ujenzi wa bomba la mafuta ghafi wa jumla ya Kilometa 1,443 kutoka magharibi mwa Uganda hadi kwenye bandari ya Tanga katika bahari ya Hindi, Tanga.

Chanzo: mtanzania.co.tz