Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania na Ubelgiji zakubaliana maendeleo sekta ya nishati

Tanzania Na Ubelgiji Zakubaliana Maendeleo Sekta Ya Nishati.png Tanzania na Ubelgiji zakubaliana maendeleo sekta ya nishati

Wed, 4 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dk Doto Biteko na Waziri wa Nishati wa Ubelgiji, Tinne Van Straeten wamekubaliana kishirikiana katika sekta hiyo hususani matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Katika kikao cha viongozi hao kilichofanyika Windhoek, Namibia, viongozi hao walikubaliana kutekeleza kampeni ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa maendeleo ya Afrika.

Kikao hicho kilifanyika wakati wa Mkutano wa Nchi za Africa zilipokutana kujadili matumizi ya Hydrojen katika kuzalisha umeme.

Dk. Biteko amesema ili kupata maendeleo ya kweli, Tanzania inatoa kipaumbele katika matumizi ya nishati ambayo itawawezesha kupata maendeleo endelevu ikiwa ni pamoja kuondokana na magonjwa na vifo vinavyotokana na matumizi ya nishati isiyokuwa safi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live