Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania na Malawi kushirikiana uhusiano biashara

Malawi Tanzaniaaaa (600 X 419) Tanzania na Malawi kushirikiana uhusiano biashara

Thu, 27 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tanzania na Malawi zimekubaliana kukuza uhusiano wa kibiashara na uwekezaji kwa kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara na uwekezaji.

Makubaliano hayo yanahusisha uboreshaji wa sheria za uwekezaji, ukamilishaji wa ujenzi wa Kituo cha Pamoja cha Kasumulo na huduma za bandari ya Mbamba Bey, ili kukuza biashara na uchumi baina ya nchi hizo.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah, alipokuwa akihutubia Kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Malawi linalofanyika Mzuzu, Malawi.

Aidha, amesema Tanzania inawakaribisha wawekezaji na wafanyabiashara kutoka Malawi kuwekeza na kufanya biashara Tanzania katika sekta mbalimbali ambazo ni pamoja na kilimo, uvuvi, uchumi wa bluu, uzalishaji, utalii, huduma za fedha, uchukuzi, miundombinu, mawasiliano, madini, elimu na afya.

Dkt. Hashil Abdallah pia amewataka wafanyabishara na wawekezaji wa Tanzania kutumia kikamilifu fursa zinazopatikana katika nchi hizo mbili ili kuongeza kasi ya ukuaji wa biashara ambayo kwa takwimu za mwaka 2022 ilifikia Dola Milioni 86.7 za Kimarekani.

Naye Waziri wa Biashara na Viwanda wa Malawi, Simplex Chithyola Banda amesema nchi hiyo iko tayari kuimarisha uhusiano wa kibiashara na uwekezaji na Tanzania.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live