Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania na Japan zaingia mkataba wa Bil. 174

TANZANIA NA JAPAN Tanzania na Japan zaingia mkataba wa Bil. 174

Thu, 27 Apr 2023 Chanzo: Azam TV

Tanzania na Japan kupitia Shirika lake la Ushirikiano wa Kimataifa JICA, zimetiliana saini mikataba mitatu ya mkopo nafuu na msaada wenye jumla ya Yen bilioni 10.15 sawa na shilingi za Tanzania bilioni 174.8.

Mkopo huo nafuu na msaada ni kwaajili ya kuendeleza kilimo na uvuvi, ambapo katika sekta ya kilimo, mkopo huo utatumika kununua pembejeo za kilimo ikiwemo mbolea, utoaji wa mbegu bora na kuongeza uzalishaji wa mazao ya mpunga, ngano na alizeti.

Sekta ya uvuvi itanufaika na msaada utakaotumika kufufua Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO) kwa kununua meli ya kisasa ya uvuvi na miundombinu ya kuhifadhi samaki.

Chanzo: Azam TV