Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan Pamoja na Rais wa DR Congo Felix Tshishekedi kwa pamoja wameazimia kuondoshwa kwa vikwazo vilivyopo ili kukuza biashara na uwekezaji hususani katika kuboresha miundombinu ya reli na ujenzi wa bandari wakijadili pia uwekezaji katika mawasiliano.
Hayo yameainishwa ikiwa ni matokeo ya ziara ya awali ya Rais Samia nchini Congo na hii iliyofanywa leo na Rais wa Congo nchini Tanzania ambapo kupitia tume ya pamoja ya ushirikiano maazimio 50 yameafikiwa kufanyiwa utekelezaji lengo ikiwa kuinua biashara kati ya mataifa hayo mawili.
Ziara hiyo imebainisha uwekezaji mkubwa unaofanywa na sekta binafsi katika sekta ya kilimo ili kuhakikisha uhakika wa chakula mara baada ya mataifa mengi ya afrika kupita katika ukame na majanga ya maradhi n vita vya mataifa makubwa.
Mhe Rais Felix hii Leo amekamilisha Ziara hiyo na kurejea nchini kwake akisisitiza utekelezaji wa makubaliano na Mwenyeji wake Rais Samia Suluhu Hassan.