Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania mwenyeji mkutano wa mawaziri wa Utalii Afrika

Unto.jpeg Dkt Ndumbaro akisaini Mkataba wa makubaliano ya wenyeji (Host Agreement)

Tue, 8 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

WAZIRI wa Maliasili na Utalii Dk.Damas Ndumbaro ametia saini mkataba wa uenyeji (Host Agreement), kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kuwa mwenyeji wa Mkutano wa 65 wa Mawaziri wa Utalii kwa Kamisheni ya Afrika (65th United Nations World Tourism Organization Regional Commission for Africa), utakaofanyika tarehe 5 hadi 7 Oktoba 2022, mjini Arusha.

Sherehe za utiaji saini zimefanyika Machi 7 mwaka huu katika makao makuu ya Shirika la Utalii Duniani (UNWTO) na kuhudhuriwa pia na Ubalozi unaowakilisha wa Ufaransa unaowakilisha pia Uhispania na UNWTO.

Kabla ya utiaji saini, ujumbe wa Tanzania ulioongozwa na Ndumbaro pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa na Uhispania Samwel W. Shelukindo kilifanyika kikao na kujadili maeneo mbalimbali ya ushirikiano.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live