Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania mwenyeji mkutano wa korosho, nchi 33 kushiriki

Mwenyeji Korosho Tanzania mwenyeji mkutano wa korosho, nchi 33 kushiriki

Sat, 15 Jul 2023 Chanzo: Mwananchi

Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano wa kimataifa wa zao la korosho utakaohudhuriwa na wasihiriki 500 kutoka zaidi ya nchi 33, ambapo fursa mbalimbali zitokanazo na zao hilo zitatangazwa kwa wadau mbalimbali.

Akizindua uandikshaji wa washriki wa mktano huo, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho Tanzania (CBT), Francis Alfred, amesema kuwa mkutano huo utafanyika kuanzia Oktoba 11-13 ambao una lengo la kutangaza fursa mbalimbali zitokanazo na zao la korosho.

“Katika mkutano huu tutahamasisha matumizi ya korosho na bidhaa zake ndani ya nchi kama vile mafuta ya ganda la korosho, shurubati (juice), maziwa ya korosho, mvinyo, nyama ya bibo na pombe kali,” amesema na kuongeza;

“Zipo bidhaa nyingi kama Ethanol zinaweza kutumika kwenye maabara za hospitali na shule zetu na hivyo kupanua wigo wa soko la korosho.”

Amezitaja nchi zitakazoshiriki katika mkutano huo ambazo zinalima zao hilo kuwa ni Ivory coast, Cambodia, India, Vietnam, Brazil, Indonesia, Sri Lanka, Nigeria, Guinea Bissau, Burkina Faso, Mali, Benin, Ghana, Madagascar, Zambia, Msumbiji, Kenya, Mauritius, Visiwa vya Comoro na wenyeji Tanzania.

Pia watashiriki wadau mbalimbali kutoka nchi ambazo ni walaji wa korosho ikiwa ni pamoja na Marekani, nchi za ulaya, China, Arabuni, Mashariki ya Kati, lakini pia Afrika Kusini pamoja na nchi nyingine za bara la Afrika.

“Mkutano huo unakusudia kuwa na washirki wote walioko katika mnyororo wa thamani wa tasnia ya korosho kama vile wakulima, wabanguaji, wasindikaji, wakaangaji, wasafirishaji, vyama vya ushirika, na wasambazaji wa pembejeo,” amesema na kuongeza;

“Wadau wengine wataohudhuria ni waendesha maghala, watafiti, wazalishaji wa mitambo na vipuli, wasimamizi wa tasnia, walaji au watumiaji wa bidhaa za korosho, taasisi za fedha, watunga sera, wawekezaji, wabia wa maendeleo na wadau wengine wengi.”

Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo amesema kuwa taarifa ya hali ya uchumi ya mwaka 2022, inaonyesha zao la korosho lilichangia zaidi ya dola milioni 226. 9 kwenye pato la taifa (GDP).

“Katika ubanguaji kuna matarajio ya kuongezeka kwa viwanda vya kubangua na kusindika korosho na bidhaa zake na kuimarika kwa masoko kwa kufungua masoko ya korosho na bidhaa zake ndani na nje ya nchi,” amesema.

Chanzo: Mwananchi