Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania mwenyeji Mkutano Usalama wa Anga

ATCL Kupunguza Safari Za Ndege Tanzania mwenyeji Mkutano Usalama wa Anga

Fri, 12 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkutano wa Sita wa Taasisi inayosimamia Ulinzi na Usalama wa Usafiri wa Anga Afrika Mashariki (CASSOA) unatarajia kufanyika Zanzibar kuanzia Mei 15 hadi 16 2024.

Mkutano huo utawakutanisha wadau muhimu wa Usafiri wa Anga ikiwa ni pamoja na makampuni ya ndege, viwanja vya ndege, wasimamizi na wadau wa usalama katika sekta ya anga kutoka nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo pia wajumbe watajadili maswala ya utunzaji wa mazingira.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Hamza Johari amesema mikutano ya EAC Aviation ilianzishwa na Bodi ya EAC-CASSOA kama njia ya kuongeza uelewa juu ya maswala yanayoathiri Usalama wa Usafiri wa Anga katika kanda yetu wa Africa Mashariki na Duniani kwa ujumla.

Amesema malengo ya Mkutano wa sita wa EAC -CASSOA ni kuchunguza na kurejesha upya tasnia ya anga na kurudisha imani ya watumiaji, kuongeza uelewa wa fursa zinazohusiana na ubunifu wa sasa wa anga, kujadili masuala endelevu ya mazingira katika anga na Kubadilishana maarifa

Amesema kauli mbiu ya Mkutano wa sita wa EAC wa Usafiri wa Anga ni "Hatima ya Usafiri wa Anga: Kudumisha mifumo ya anga iliyo imara, endelevu, ya ubunifu, salama na yenye usalama."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live