Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania kuwania fursa hii Zambia

Bandari Chachamaa Tanzania kuwania fursa hii Zambia

Fri, 5 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali ya Zambia imeeleza nia yake ya kuendeleza ushirikiano na nchi jirani katika usafirishaji wa shehena kutoka na kuingia nchini humo ili kukuza uchumi wa nchi hiyo na kutumia vyema fursa zilizopo hasa katika rasilimali za madini.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Uchukuzi na Usafirishaji wa Zambia, Frank Tayali wakati akifungua kongamano la tatu la Biashara na Usafirishaji (Land-Linked Zambia Transport and Logistics event) Jijini Lusaka nchini Zambia.

Akizungumza kando ya kongamano hilo kwa niaba ya Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa, Balozi wa Tanzania nchini Zambia, Luteni Jenerali Mathew Mkingule, amesema kongamano hilo ni muhimu katika kuitangaza Tanzania kupitia miundombinu wezeshi.

Naye mwakilishi wa TPA nchini Zambia, Hamisi Chambari aliyezungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TPA amesema kuwa TPA ina nafasi muhimu katika kongamano hilo kama mdau muhimu katika sekta ya uchukuzi ikihudumia nchi kadhaa za SADC ikiwemo Zambia.

TPA inashiriki kongamano hilo la siku mbili lililoanza leo Aprili 4, 2024 likihusisha taasisi za Sekta ya Uchukuzi kwa Ukanda wa nchi za Kusini mwa Afrika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live