Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania kuwa mwenyeji mkutano wa kimataifa wa Utalii

Utalii Kifo Mkutano huo utakaofanyika jijini Arusha Oktoba 5 hadi 7, 2022

Sat, 21 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tanzania inatarajia kuwa mwenyeji wa mkutano wa kimtaifa utalii wa Shirika la Utalii Dunia (UNWTO) Kamisheni ya Afrika ambao unalenga kujadili za namna ya kuiimarisha sekta ya utalii Afrika ili kuhimili majanga mbalimbali ikiwemo ugonjwa wa Corona (Uviko-19).

Mkutano huo utakaofanyika jijini Arusha Oktoba 5 hadi 7, 2022 unatarajiwa kuhudhuriwa na mawaziri wa utalii a uhifadhi wanachama wa UNWTO na kufuatiwa na jukwaa la wazi kujadili kwa kina na kutoka na mapendekezo ya namna ya kujenga upya ustahimilivu wa utalii wa Afrika kwa maendeleo jumuishi ya kijamii na kiuchumi.

Huenda mapendekezo hayo yakasaidia kuimarisha sekta ya utalii Afrika kwa kuongeza idadi ya watalii na mapato baada ya Uviko-19, igonjwa ambao uliwafanya watu wengi kukosa kazi na kupungua kwa uhifadhi wa maliasili na bidhaa zinazotumika katika utalii.

Ili kufanikisha mkutano huo, Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dk Francis Michael amezinduwa rasmi kamati ya kitaifa ya maandalizi ya mkutano huo wa 65 (65th UNWTO-CAF MEETING).

“Nategemea kamati hii itafanya kazi kwa weredi, maarifa na kuwa na kasi kubwa katika maandalizi haya,” amesema Dk Michael.

Amesema yupo tayari kushirikiana na kamati hiyo ili Tanzania iwe mfano kwa nchi nyingine wananchama wa umoja huu.

“Nina nafasi ya kufanya mabadiliko ya wajumbe wakati wowote pale ninapoona maandalizi yanalegalega”, amesema Dk Michael Mei 19, 2022 wakati wa uzinduzi wa kamati hiyo uliofanyika jijini Arusha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live