Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania kuwa kitovu uchakataji madini Afrika

Madini Pic Data Tanzania kuwa kitovu uchakataji madini Afrika

Tue, 22 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Imeelezwa kuwa, Serikali inaandaa Mkakati wa kuwezesha uongezaji thamani madini kwa lengo la kuzalisha bidhaa mbalimbali zinazotokana na madini utakaopelekea Tanzania kuwa kitovu cha uchakataji madini kwa lengo la kuvutia wawekezaji wa ndani na nje. - Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa wakati akifungua rasmi Maonesho ya Madini na Fursa za Uwekezaji yanayokwenda sanjari na Kongamano la Wadau wa Madini ya Chumvi Mkoani Lindi leo Agosti 21, 2023 - Aidha amesema, Serikali imeendelea kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji na biashara nchini ili kuvutia mitaji kutoka ndani na nje ya nchi, amesema katika kutekeleza azma hiyo, Serikali imeendelea kufanya mapitio ya Sera mbalimbali zinazosimamia Uwekezaji, Viwanda na Biashara nchini.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Lindi Zainabu Telack amesema kuwa kupitia maonesho haya wawekezaji wanajionea fursa mbalimbali za rasilimali madini ikiwa pamoja na kutangaza fursa nyingine za kiuchumi zinazopatikana mkoani Lindi.

Kaulimbiu ya maonesho hayo ni "Wekeza Lindi kwa Ukuaji wa Uchumi wa Maendeleo ya Jamii". Maonesho hayo yamehudhuriwa na wadau mbalimbali wa Sekta ya Madini waliopo ndani na nje ya nchi yanayoendelea hadi Agosti 26 mkoani Lindi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live