Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania kuvuna fursa uenyekiti wa kamisheni ya wanyamapori Afrika

Gjhkjuhoin.png Tanzania kuvuna fursa uenyekiti wa kamisheni ya wanyamapori Afrika

Thu, 2 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwenyekiti mpya wa kamisheni ya misitu na wanyapori barani Afrika (AFWC24), Prof Dos Santos Silayo amesema kuwa Tanzania haitafanya makosa katika nafasi hiyo.

Tanzania imechaguliwa kuwa mwenyeji wa ofisi ya kamisheni ya 24 ya misitu na wanyama pori barani Afrika (AFWC24) kwa kipindi cha miaka miwili kuanzia mwaka 2023 hadi 2025.

Tanzania imepitishwa uenyeji huo kwenye mkutano wa AFWC24 unaoendelea jijini Arusha huku Kamishna wa Uhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Prof Dos Santos Silayo ndio amechaguliwa kuongoza kamisheni hiyo.

"Akizungumzia nafasi hiyo leo Novemba 2, 2023 Prof Silayo amesema kuwa Tanzania kupata nafasi hiyo haitafanya makosa bali itatumia fursa kuhakikisha nchi inanufaika.

"Uenyeji huu ni muhimu sana kwa nchi yetu, hivyo hatutatumia nafasi hii vibaya, tatahakikisha hakuna fursa inatupita," amesema.

Aidha kwa upande wa nafasi ya makamu wa kwanza wa mwenyekiti, Tanzania imepokewa na Mali, huku makamu wa pili ya uenyekiti imeshikwa na Malawi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live