Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania kuuza umeme nje ya nchi

Mgawo Wa Umeme No Tanzania kuuza umeme nje ya nchi

Tue, 30 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Nishati January Makamba amesema ndoto ya Tanzania kuuza umeme nje ya Nchi bado ipo lakini ni lazma kwanza Serikali ijiridhishe kwenye mambo kadhaa kabla ya kuuza.

Akiongea kwenye Maonesho ya Wiki ya Nishati Jijini Dodoma Makamba amesema “Ili kutimiza ndoto ya kuuza umeme nje, kwanza ni lazima umeme wetu uwe umejitosheleza kwa Watu wetu wa ndani, pili Kujenga inter connector ambapo kwa sasa vitu vyote hivyo viwili bado havijakamilika”

“Ushiriki wa Sekta binafsi kwenye Sekta ya Nishati ni kipaumbele chetu, tunawaza badala ya kuchukua hela hazina kwa ajili ya kujenga mtambo wa umeme, tutasema wewe jenga mtambo kwa hela yako kisha sisi tutanunua kwako umeme, hapo wote tutapata faida huo ndo uwekezaji tunaozungumzia kwenye Sekta binafsi ili hizi hela za Serikali zikasaidie mambo mengine kama dawa Hospitalini”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live