Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania kuuza fursa za biashara EU

Dkt Phillip Mpango Xmass.jpeg Tanzania kuuza fursa za biashara EU

Thu, 23 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango leo anatarajiwa kumwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan katika ufunguzi wa kongamano la biashara na uwekezaji jijini Dar es Salaam.

Kampuni 600 za ndani na nje zinatarajiwa kushiriki kongamano hilo zikiwamo 400 kutoka nchi za Umoja wa Ulaya (EU) na 200 za Tanzania.

Kongamano hilo limeandaliwa kwa ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania, EU na Taasisi ya Sekta ya Binafsi Tanzania (TPSF) kwa lengo la kuangalia fursa za biashara na uwekezaji zilizopo nchini.

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Dk Ashatu Kijaji, hivi karibuni alivieleza vyombo vya habari Dar es Salaam kuwa hati za makubaliano ya uwekezaji na biashara na mikataba ya fedha kati ya Tanzania na nchi za EU zitasainiwa.

Pia Dk Kijaji alisema kongamano hilo litahudhuriwa na mawaziri wanane kutoka Serikali ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar pamoja na mabalozi sita wa Tanzania katika nchi za Umoja wa Ulaya.

Matarajio makubwa ya Tanzania na Watanzania katika kongamano hili ni kuona linavutia wawekezaji, teknolojia na utaalamu kuja nchini pamoja na kuvutia biashara na uwekezaji kutoka duniani kote katika sekta za nishati, madini na kilimo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live