Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania kutumia fursa za biashara Afrika

7dcc4412e975b91723cc3fc0162bd29a Tanzania kutumia fursa za biashara Afrika

Thu, 1 Jul 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

RAIS Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania ipo kwenye hatua za mwisho kuridhia Mkataba wa Eneo Huru la Biashara Afrika (AfCFTA).

Taarifa ya Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Jaffar Haniu ilieleza kuwa Rais Samia alisema hayo jana Ikulu ya Chamwino Dodoma alipokutana na kuzungumza na Katibu Mtendaji wa Sekretarieti ya AfCFTA, Wamkele Mene.

Rais Samia alimpongeza Mene kwa kushinda nafasi hiyo ya uongozi AfCFTA na akamhakikishia kuwa Tanzania itashirikiana nae kufanikisha utendaji kazi wake ili kulikwamua Bara la Afrika kiuchumi.

Taarifa ya Haniu kwa vyombo vya habari ilieleza kuwa Mene alimpongeza Samia kuwa Rais wa kwanza mwanamke Tanzania na Rais pekee mwanamke ambaye ni mkuu wa nchi na serikali barani Afrika.

Mene aliishukuru Tanzania kwa kurejea kwenye majadiliano na masuala mengi waliyojadili wamekubaliana.

Alimualika Rais Samia ahudhurie mkutano wa sekretarieti jijini Accra, Ghana na awe Mzungumzaji Mkuu kwenye mkutano huo wenye lengo la kuandaa Itifaki ya Wanawake katika Biashara.

Kupitia mkutano huo kwa ajili wa wafanyabiashara ndogondogo sekretarieti inatarajia kufanya harambee ya kukusanya fedha kutoka taasisi za fedha na benki kwa ajili ya kuwezesha biashara.

Mene alimhakikishia Rais Samia kuwa sekretarieti ya AfCFTA inakusudia kuhakikisha wanachama wake wote wananufaika kwa usawa kupitia uwekezaji katika viwanda ambavyo vitaongeza minyororo ya thamani ya bidhaa zinazozalishwa katika nchi wanachama.

Alimpongeza Rais Samia kwa kuirudisha Tanzania katika dhima yake ya uongozi kama alivyowahi kufanya Baba wa Taifa Mwl. Julius Nyerere ambaye alikuwa muasisi wa Umajumui wa Afrika.

Chanzo: www.habarileo.co.tz