Waziri wa Maliasili na Utalii Angellah Kairuki amekutana na kufanya mazungumzo na Rais ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Utalii Duniani Julia Simpson, kwa lengo la kujadili namna bora ya kushirikiana katika kutangaza na kukuza utalii endelevu nchini Tanzania.
Mkutano huo umefanyika kwenye hoteli ya Seasons jijini Riyadh, Saudi Arabia.
Aidha, katika kuendelea kutangaza utalii na kutafuta masoko mapya ya utalii, Waziri Kairuki amefanya mazungumzo na wadau wakubwa wa utalii duniani ikiwa ni pamoja na Meneja Masoko wa Shirika la Ndege la Saudi Arabia, Abdulrahman Alabdulwahab ili kuangalia namna bora ya kuitangaza Tanzania kupitia ndege za shirika hilo na kushirikiana katika kutangaza vivutio vya Utalii nchini.