Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania kushiriki mkutano wa madini

Mavunde Atoa Mwelekeo Mpya Sekta Ya Madini Tanzania kushiriki mkutano wa madini

Mon, 22 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wizara ya Madini imesema kuwa kwa mara ya kwanza kwa kushirikiana na Chemba ya Migodi inayowakilisha Sekta Binafsi zitashiriki kwa pamoja kuiwakilisha Tanzania katika Mkutano wa Madini Barani Afrika wa "Mining Indaba" unaofanyika mwezi Februari kila mwaka nchini Afrika Kusini.

Mkutano huo utafanyika tarehe 5 hadi 8 Februari, 2024 katika jiji la Cape Town ukiwa ni sehemu muhimu ya kujenga uhusiano na kuongeza wigo wa kibiashara katika sekta ya madini. Pia, umeendelea kutumika kama eneo la kutafuta wawekezaji, mitaji, teknolojia, wabia, biashara, kubadilishana uzoefu na kujifunza kuhusu usimamizi endelevu na ukuzaji wa Sekta ya Madini Barani Afrika.

Tanzania itashiriki chini ya kaulimbiu "Ustawi Imara kwa Kuendeleza Uwekezaji katika Sekta ya Madini,” Kaulimbiu hii inachochea jitihada za Serikali ya Tanzania kutekeleza vipaumbele vya Wizara katika kuendeleza madini muhimu na mkakati ikiwemo Dira ya 2030: Madini ni Maisha na Utajiri", inayolenga kupata taarifa za kina za kijiofizikia kufikia asilimia 50 ya nchi yetu kutoka asilimia 16 ya sasa.

Aidha, uongezaji thamani madini ni eneo lingine la kipaumbele kwa Tanzania ili kuhamasisha ujenzi wa viwanda vya kuchenjua, kuyeyusha na kuongeza thamani madini na kuhakikisha shughuli hizo zote zinafanyika nchini ili kuongeza thamani ya madini yanayozalishwa nchini, kuongeza mapato yatokanayo na shughuli za madini na kupanua wigo wa ajira.

Tanzania katika mkutano huo imejikita katika kuendelea kutangaza na kuhamasisha fursa za kiuwekezaji zilizopo katika sekta ya madini nchini.

Fursa zimejikita katika utafutaji, uchimbaji, uchenjuaji na uongezaji thamani madini pamoja na dhamira ya Serikali ya kuboresha mazingira ya biashara ya madini zikiwemo Sheria na Kanuni, zinazosimamia shughuli za madini nchini, uendelezaji wa rasilimali watu ili kuwa na usimamizi madhubuti wa sekta ya madini na kuhamasisha ubia wenye manufaa kwa pande zote.

Katika mkutano huo, Tanzania imepata nafasi ya kuwa na siku maalum ya kukutana na wadau mbalimbali ambapo itapata wasaa wa kutoa wasilisho na kutangaza fursa zake za uwekezaji na biashara ya madini zilizopo nchini. Hivyo, mkutano huo ni fursa adhimu ya kuichumi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live