Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania kupeleka intaneti Burundi

81229 TTCL+PIC Tanzania kupeleka intaneti Burundi

Tue, 22 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limesaini mkataba na kampuni ya  mawasiliano ya mkongo wa Taifa ya Burundi (BBS) kwa ajili ya kupeleka huduma ya intaneti nchini humo.

Mkataba huo wa Sh13.8 bilioni utatekelezwa katika nchi ya Burundi kwa kipindi cha miaka 10.

Makubaliano hayo yamesainiwa leo Jumanne Oktoba 22, 2019 nchini Tanzania na mtendaji mkuu wa TTCL, Waziri Kindamba na ofisa mtendaji mkuu wa BBS, Elie Ntihagowumwe.

Akizungumza baada ya kusaini mkataba huo,  Kindamba amesema TTCL itatoa mawasiliano ya uhakika katika nchi hiyo.

Amebainisha kuwa kupitia mkataba huo Serikali imeongeza mapato na wigo wa biashara katika nchi za Afrika Mashariki na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (Sadc).

"TTCL itatoa huduma ya mawasiliano ya mkongo wa Taifa nchini Burundi kupitia vituo vyetu vya mpakani katika miji ya Kabanga na Manyovu na kuiunganisha nchi hiyo na dunia kupitia mikongo mikubwa ya baharini.”

Pia Soma

Advertisement

“Makubaliano haya yametanua wigo wa kutoa huduma na tunategemea kuongeza huduma kutoka 2.5 GBPS ya sasa mpaka kuwa 10GPS,” amesema Kindamba.

Kindamba ameainisha huduma za mawasiliano zitakazotolewa na TTCL kupitia makubaliano hayo kuwa ni data na intaneti.

Nyingine ni utunzaji wa kumbukumbu mbadala kupitia kituo cha kimataifa cha kutunza kumbukumbu kilichopo nchini, kubadilishana wataalamu na wahandisi, kuwajengea uwezo wa kitaalamu katika nyanja za mawasiliano.

" Pia tutabadilishana wateja wakubwa wenye matawi na ofisi za biashara mfano benki ya CRDB, kupeana ushauri wa kitaalamu kuhusu watoa huduma na watengenezaji wakubwa wa vifaa vya mawasiliano vinavyotumika katika mawasiliano,” amefafanua.

Mpaka sasa TTCL imewafikia wateja zaidi ya milioni 2  huku wanaotumia huduma ya T Pesa wakifikia 600,000 nchi nzima.

"Pia tuna mawakala 19,000 nchi nzima na miamala ya takribani Sh5 bilioni imeshatolewa,” amesema.

Naye Ntihagomumwe  amesema huduma hiyo itawanufaisha wananchi kwa kuwawezesha kutekeleza vizuri shughuli zao zinazohusu Tehama.

" Mbali na wananchi wa Burundi kunufaika na huduma hii, pia BBS itajifunza vitu vingi kutoka TTCL,” amesema.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz