Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania kunufaika na mabilioni ya Italia

Pesa Fedhaddd Tanzania kunufaika na mabilioni ya Italia

Mon, 29 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tanzania imechaguliwa kuwa moja ya nchi nane za Afrika zitakazopewa kipaumbele na Italia kupitia mpango mpya wa kimkakati wa Mattei (Mattei Plan) ambapo Euro Bilioni tano za awali zimetengwa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hiyo.

Miradi hiyo ya kipaumbele kupitia Mpango mpya wa Kimkakati wa Mattei ipo katika sekta ya nishati, elimu na kilimo.

Taarifa hiyo imetolewa na Rais wa Chama cha Wafanyabiashara wa Italia Mhandisi Alfredo Cestari alipokutana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki January Makamba pembezoni mwa mkutano wa nne wa Wakuu wa Nchi za Afrika na Italia unaoendelea Roma,Italia.

Utekelezaji wa mpango huo utaanza mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa Wakuu wa nchi za Afrika na Italia ambapo Serikali ya nchi hiyo itafadhili miradi ya kipaumbele kwa nchi nane za awali za Afrika.

Hatua hiyo itahusisha pia gharama za upembuzi yakinifu ya miradi itakayopendekezwa.

Kama hatua ya utekelezaji ya mpango huo, ujumbe wa wataalam kutoka Chemba ya Biashara ya Italia ikiongozwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Dkt. Edmondo Cirielli unatarajiwa kuwasili Tanzania ndani ya kipindi cha mwezi mmoja kwa ajili ya kukutana na timu ya wataalam ya upande wa Tanzania kwa ajili ya kukamilisha hatua za awali za utiaji saini wa ushirikiano huo wa pande mbili utakaohusisha utekelezaji wa miradi itakayopitishwa na pande mbili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live