Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania kunufaika na fursa za Qatar

Maji Maji Majaliwa yuko ziarani mashariki ya kati

Fri, 25 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Huenda Watanzania wakaendelea kufaidika na biashara ya kimataifa hasa inayofanywa kati ya Tanzania na Qatar baada ya viongozi wa nchi hizo mbili kukutana ili kujadili namna ya kukuza ushirikiano katika sekta mbalimbali.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Qatar, Sheikh Khalid bin Khalifa bin Abdulaziz Al Thani ambapo wamekubaliana kuimarisha ushirikiano katika sekta mbalimbali ikiwemo biashara ili kukuza uchumi.

“Ninamuwakilisha Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan katika vikao vyenye lengo la kuimarisha mahusiano kati ya nchi ya Tanzania na Qatar na tumepata fursa ya kukutana na viongozi mbalimbali ikiwa ni muendelezo wa ushirikiano kati ya nchi ya Tanzania na Qatar,” amesema Majaliwa.

Majaliwa ametoa kauli hiyo wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Qatar, Sheikh Khalid bin Khalifa bin Abdulaziz Al-Thani, Doha,Qatar.

Amesema moja kati ya jambo kubwa walilolijadili ni uimarishwaji wa tume ya pamoja ya ushirikiano ili kuongeza wigo wa maeneo mengi zaidi ya ushirikiano baina ya mataifa hayo na hivyo kutumia vema fursa ya kuwa na ushirikiano mzuri wa kidiplomasia wa miaka mingi.

Waziri Mkuu amesema kuwa kati ya mambo waliyoyawekea msisitizo ni pamoja na kuimarisha biashara kupitia Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) na Chemba ya Biashara ya Tanzania kupitia ushirikiano na wenzao wa Qatar na kwamba shughuli hizo zitaratibiwa na wizara husika ili kuhakikisha makubaliano hayo yanatekelezwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live