Waziri wa Madini, Dkt. Doto Biteko amesema kuwa, Serikali iko mbioni kuanzisha upya Minada ya Madini ya Vito ili kuleta wanunuzi wakubwa, wafanyabiashara na wachimbaji wa madini hapa nchini.
Hayo yamebainishwa Januari 5, 2023 wakati akizindua duka la utalii wa madini la kampuni ya Tanzanite Experience katika eneo la Manyara Kibaoni wilaya ya Karatu Mkoani Arusha
Amesema kupitia mnada huo kampuni ya Tanzanite Experience kupitia duka la utalii wa madini itapata madini mengi kwa ajili ya kuendeleza kituo hicho na maeneo mengine anayoyafanyia kazi.
Dkt. Biteko amesema kuwa, kupitia kituo hicho kilichopo katika ukanda wenye maeneo ya hifadhi imekuwa ni sehemu kubwa ya kivutio cha utalii kwa wageni kutoka ndani na nje ya nchi.