Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania kivutio cha kwanza utalii Afrika

152f356e0058a14b8b86c4d5bc9c7674 Tanzania kivutio cha kwanza utalii Afrika

Sat, 4 Jun 2022 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Tanzania imekuwa kivutio cha kwanza cha utalii barani Afrika katika kipindi cha mwaka huu.

Hayo yalibainishwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Pindi Chana, wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake bungeni jana kwa mwaka ujao wa fedha 2022/2023.

Balozi Chana alisema mtandao maarufu wa habari nchini Marekani ujulikanao kama theGrio umetambua juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan katika kuiongoza sekta ya utalii na uhifadhi nchini, hivyo kuifanya Tanzania kuwa kivutio cha kwanza cha utalii katika bara hili.

Pia alisema serikali ilisaini mkataba wa ushirikiano katika masuala ya utalii, bi-ashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Jiji la Dallas nchini Marekani mwezi Aprili mwaka huu jambo litakalosaidia kufungua fursa za usafiri wa anga wa mo-ja kwa moja kutoka Tanzania hadi Dallas, Marekani na kuongeza idadi ya wageni hapa nchini.

“Jitihada hizi zitaleta matokeo chanya katika kuongeza idadi ya watalii na ku-fikia lengo la watalii milioni tano na mapato Dola za Marekani bilioni sita ifikapo mwaka 2025,” alisema.

Kuhusu filamu ya Tanzania Royal Tour, alisema filamu hiyo imeitambulisha Tanzania kimataifa kwa kutangaza vivutio vya utalii, kuonesha fursa za uwekezaji kwenye sekta ya maliasili na utalii pamoja na kuimarisha nafasi ya nchi katika jumuiya za kimataifa.

Alisema filamu hiyo pia inaonesha vi-vutio vya utalii katika hifadhi za Taifa, Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro, maeneo ya malikale, tamaduni za Kitanzania na visiwa vya Zanzibar.

Kwa mujibu wa Chana, matunda ya filamu hiyo yameanza kuonekana ikiwemo kuvutia watalii na wawekezaji hapa nchini wakiwemo wakala wa utalii zaidi ya 30 kutoka masoko ya utalii ya Marekani, Ufaransa na Lithuania.

Aliongeza kuwa wawekezaji kutoka nchini Bulgaria nao wameonesha nia ya kuwekeza hapa nchini kwa kujenga hoteli nne zenye hadhi ya nyota tano katika hifadhi za Taifa Serengeti, Ziwa Manyara, Tarangire na eneo la Hifadhi ya Ngorongoro.

Katika kuchochea matokeo chanya ya fil-amu hiyo, Chana alisema wizara yake itaimarisha miundombinu ya utalii ikiwemo barabara, viwanja vya ndege na mawasiliano katika maeneo ya hifadhi ili kuhakikisha vivutio vilivyomo vinafikika kwa urahisi.

Pia itaboresha huduma za malazi kwa kuongeza idadi ya vitanda, kuvutia uwekezaji, kutangaza vivutio vya utalii, kuibua mazao mapya ya utalii, kuimarisha utoaji mafunzo ya huduma katika sekta ya utalii na ukarimu, kuimarisha ulinzi na usalama wa wageni wanaotembelea hifadhi pamoja na kuimarisha ushirikiano na wadau ikiwemo sekta binafsi.

Kwa mujibu wa Balozi Chana, utalii unachangia asilimia 25 ya fedha za kigeni na huzalisha ajira takribani milioni 1.6 za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja kwa mwaka.

Chanzo: www.habarileo.co.tz