Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania kinara uchumi jumuishi ikifanya vizuri pesa mtandao

Uchumi Kupanda Tanzania kinara uchumi jumuishi ikifanya vizuri pesa mtandao

Tue, 20 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kutokana na utafiti uliofanywa na Shirika la kimataifa linalounganisha mfumo ikolojia wa simu ili kugundua, kuendeleza na kutoa ubunifu unaosaidia biashara na jamii kustawi (GSMA) umeonyesha kuwa Watanzania wengi nchini hawajaunganishwa Pesa Mtandao (Mobile Money).

Akiwasilisha yaliyomo kwenye utafiti huo Mkurugenzi wa Sera za Kijamii, Kusini mwa jangwa la Sahara, Caroline Mbugua amesema Tanzania imeonekana kuwa na ushuru mkubwa karibu mara mbili ya nchi zilizo Kusini mwa jangwa la Sahara ikiwa na asilimia 47 kwenye Pesa Mtandao.

Hata hivyo Tanzania imefanya vizuri kwenye uchumi jumuishi ikifanya vizuri kwenye Pesa Mtandao.

Ni asilimilia 52 pekee ya Watanzania (watu wazima) wanaotumia pesa mtandao chini zaidi ikilinganishwa na Uganda asilimia 66, Kenya asilimia 79 na Afrika Kusini asilimia 85.

GSMA imependekeza kuondolewa kwa makato kwenye pesa mtandao ili kuchochea ukuaji wa uchumi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live