Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania inapoteza hekta 469,000 za misitu

PINDI WEB Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Dkt. Pindi Chana

Sun, 5 Jun 2022 Chanzo: eatv.tv

Waziri wa Maliasili na Utalii,  Balozi Dkt. Pindi Chana, amesema Tanzania inapoteza takribani hekta 469,000 za misitu kila mwaka na kusema kuwa kama juhudi za pamoja hazitachukuliwa kuna hatari ya nchi kuanza kupata athari za kimazingira ambazo huathiri nchi na Dunia kwa ujumla.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Dkt. Pindi Chana, Jijini Dodoma wakati akizindua mpango kazi wa Kitaifa wa usimamizi shirikishi wa misitu na takwimu za usimamizi shirikishi wa misitu ya jamii, na kuwataka wadau wa misitu nchini kusoma kwa makini takwimu za usimamizi shirikishi wa misitu ili kupata picha ya hali halisi.

"Ili nyaraka hizi zieleweke vyema na  kutumika kwa ukamilifu miongoni mwa wadau walio wengi, ninaiagiza idara ya misitu na Nyuki izifanyie tafsiri nyaraka hizi ziwe kwa lugha ya Kiswahili na zisambazwe kwa wadau wengi kwa kadri itakavyowezekana" amesema Balozi Chana

Aidha, amewahimiza wamiliki wa misitu ya jamii ikiwemo ya vijiji kuisimamia kikamilifu kulingana na sheria, kanuni na miongozo iliyopo akisisitiza kuwa iwapo mpangokazi aliouzindua utatekelezwa ipasavyo, utawezesha uhifadhi na matumizi endelevu misitu ya jamii na pia kuchangia maendeleo endelevu katika sekta nyingine.

Chanzo: eatv.tv