Tanzania kwa sasa inajikita katika kutumia mfumo na njia zinazotumia na Taifa la Uchina na India katika jitihada za kumaliza tatizo la uhaba wa sukari ambalo limekua likijirudia.
Mfumo huo ni ule wa kutumia kusindika miwa midogo na badae kuzalisha sukari na kusambazwa ili kukabiliana na upungufu wa sukari wa tani 300,000 zinazohitajika nchini.
Akiongea na waandishi wa Habari jana, Waziri wa Viwanda na Biashara Kitila Mkumbo amesema hatua hiyo ni mojawapo ya mipango ya utawala wa Rais Samia inayochukuliwa kuhakikisha Tanzania inajitgemea katika uzalishaji wa sukari.
"Kama tunataka kuziba pengo la upungufu wa sukari tunahitaji wasindikaji wadogo kuwasaidia wazalishaji wakubwa wa sukari" amesema Prof. Kitila
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uhandisi na Utengenezaji wa Viwanda(Temdo) Prof. Frederick Kahimba alisema wanabuni na kutengeneza mitambo ya kusindika miwa.
Kahimba alisema zoezi la kubuni na kuzalisha miwa ya kusindika lilianza mwezi machi mwaka huu na tayari wamefikia asilimia 40% na kwa 20% wamekamilisha.
"Tunatarajia kukamilisha uzalishaji wa kusindika mimea ya miwa midogo ifikapo juni mwaka 2022 kabla ya kuanza shughuli za uzalishaji mwezi July" amesema Prof. Kahimba.
Alisema kwa wasindikaji wadogo wanapaswa kuwa na milioni 250 kuweza kufanikisha zoezi la usindikaji kutoka Temdo.