Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania ina uwezo wa kuwa kinara takwimu za mizani ya chakula

Wed, 8 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) imesema kuwa, ina matumaini makubwa kuwa katika kipindi kifupi kijacho, Tanzania itakuwa kinara wa Afrika katika kuweka takwimu za mizania ya chakula.

Akizungumza  wakati wa  mafunzo ya siku tatu kuhusu namna ya kuweka takwimu za mezania ya chakula nchini, Mtaalamu kutoka Benki hiyo Vincent Ngendakumana ameeleza kuwa, wakati wa mafunzo hayo wamegundua kuwa Tanzania ina nafasi na uwezo mkubwa wa kuweka Takwimu za chakula.

“Benki ya Maendeleo ya Afrika imetoa mafunzo haya kuongeza weledi kwa wataalamu wa Tanzania wa namna ya kuweka mizania ya chakula na sina shaka yoyote si muda mrefu Tanzania itakuwa kinara na nchi nyingine zitakuja kujifunza kwake,” amesema Ngendakumana

Kwa mujibu wa mtalaamu huyo ambaye ni  Mtakwimu Mwandamizi wa Takwimu za Kilimo wa benki hiyo yenye  makao makuu yake jijini Abidjan, Ivory Coast, mafunzo hayo ni sehemu ya mpango wa dunia wa kuimarisha Takwimu za kilimo ambapo kumewekwa miongozo maalum ya kuzingatia wakati wa kuweka takwimu za mizania ya chakula.

Katika mafunzo hayo yaliyofanyika katika Ofisi mpya za NBS jijini Dodoma, mtaalamu huyo  alibainisha kuwa washiriki walijifunza miongozo hiyo pamoja na kutambua vyanzo vya Takwimu za chakula na namna ya kuzikusanya na kuzioanisha ili kupata Takwimu sahihi za mezania ya chakula wakati wote.

 “Ujio wetu hapa ni kuitikia wito wa Serikali ya Tanzania iliyoutoa mwaka 2014 kupitia Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), ambayo ilituomba kusaidia kuwajengea uwezo Wataalamu katika eneo hili” almeeleza Ngendakumana.

Amebainisha kuwa katika maombi hayo, Tanzania ilieleza kuwa ili kukabiliana na upungufu wa taarifa/Takwimu za chakula, mambo matatu yakitekelezwa tatizo hilo halitokuwepo tena na kubainisha kuwa miongoni mwa mambo hayo ni kupatiwa utalaamu katika uwekaji wa mezania ya chakula.

Maombi mengine yalikuwa katika maeneo ya uzalishaji wa takwimu za kilimo na utayarishaji wa Mpango Mkakati wa Kuimarisha Takwimu za Kilimo nchini.  

 

Chanzo: mwananchi.co.tz