Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania ina uhaba wa wahandisi kulingana na mahitaji

Gesi2 Tanzania ina uhaba wa wahandisi kulingana na mahitaji

Wed, 15 Dec 2021 Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Imeelezwa kuwa Tanzania ina uhaba mkubwa wa wahandisi, hivyo vyuo vikuu nchini vimeshauri kuongeza mitalaa itakayosaidia Serikali kutekeleza kuzalisha wataalamu hao watakaosaidia katika miradi ya maendeleo.

Hayo yamesemwa leo Jumatano Desemba 15 na    Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi Tanzania (ERB) Profesa Ninatubu Lema kwenye mhadhara uliohusisha  wahadhiri, wanafunzi na watumishi wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojiab (Must) uliolenga kujadili mchango wa wahandisi katika kutekeleza miradi ya maendeleo.

Amesema, kwa sasa Serikali imewekeza miradi mikubwa kwa ajili ya maendeleo ya Taifa kidigitali, lakini changamoto kubwa ni uhaba wa wahandisi wazawa.

''Tanzania kwa sasa ina wahandisi waliosajiliwa 31,000 hivyo bado ni idadi ndogo sana kulingana na mahitaji, hivyo ni vyema sasa vyuo vikuu viunge mkono jitihada za Serikali kuhakikisha inazalisha wataalam wa fani hiyo kwa wingi

“Ukiangalia barabara zetu, wingi wa magari zinaonyesha wazi hazitoshelezi, huku Taifa likiwekeza dola 9 milioni katika uboreshwaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo na kuonyesha kuwa fedha zipo lakini wakandarasi ni wachache,” amesema Profesa Lema.

Naye Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Aloyce Mvuma, amesema kutokana na mahitaji makubwa ya wahandisi nchini wameweka mikakati ya kuongeza ubunifu wa taaluma mbalimbali ambazo zitakuwa chachu katika kusimamia na kutekeleza miradi ya Serikalini.

Advertisement Profesa Mvuma amesema kuwa kazi ya ujenzi ni kubwa lakini changamoto ni wataalam hivyo kama chuo kinaboresha mitaala na kuongeza mitaala mwingine sambamba na kutoa nafasi kwa vijana wanaozalishwa kufanya kazi kwa vitendo.

Chanzo: www.mwananchi.co.tz