Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania ina jumla ya viwanda 13 vya magari

Kijaji 2 Ashatu Viwanda Tanzania ina jumla ya viwanda 13 vya magari

Tue, 21 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji amesema kuwa Tanzania ina jumla ya viwanda 13 vya magari, kati ya viwanda hivyo, viwanda viwili (2) vinaunganisha magari ambavyo ni GF Trucks and Equipment Ltdkilichopo Kibaha, Pwani na Saturn Corporation Limitedkilichopo Kigamboni, Dar es Salaam.

Dkt. Ashatu ameyasema hayo Leo mei 21,2024 Jijini Dodoma wakati akiwasilisha Hoja ya Bajeti ya Makadirio ya mapato na matumizi ya mwaka wa fedha 2024/2025 ya Wizara ya Viwanda na Biashara

Dkt. Ashatu amesema kuwa Viwanda 11 vilivyosalia vinatengeneza matrela huku Kiwanda cha GF Truck kina uwezo uliosimikwa wa kuunganisha magari 200 kwa mwezi na kimewekeza kiasi cha shilingi bilioni 10.752 na kimetoa ajira 300.

Aidha Ashatu amesema Mradi wa Kiwanda cha Saturn Corporation Limited umegharimu mtaji wa kiasi cha shilingi bilioni 64.3 nakina uwezo uliosimikwa wa kuunganisha vichwa vya magari 900 na tipa 270 kwa mwezi naumeajiri wafanyakazi 250.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live