Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania ina hekta milioni 14 za misitu

D85aeedbb3a97e73bceb9549aa110da5 Tanzania ina hekta milioni 14 za misitu

Mon, 29 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

WAKALA wa Misitu Tanzania (TFS), mpaka sasa unasimamia misitu 463 yenye zaidi ya hekta milioni 14, hifadhi 20 za mazingira asilia zenye hekta zaidi ya laki tisa, misitu ya mikoko hekta 145,498, na hifadhi za nyuki 12 zenye hekta 31,015.

Kamishna wa Uhifadhi TFS, Profesa Dos Santos Silayo alisema hayo alipokuwa akizungumza na HabariLEO kuhusu misitu nchini.

Profesa Silayo alisema shamba la Biharamulo ni miongoni mwa mashamba ya serikali yaliyoanzishwa na wakala huo mwaka wa fedha 2017/18 huku akieleza kuwa ukubwa wa shamba hilo ni hekta 69,756 ambalo lilianzishwa kwenye eneo lililokuwa msitu wa hifadhi Biharamulo-Kahama.

Alisema uanzishwaji wa shamba hilo la Biharamulo ulilenga maeneo yaliyoharibiwa na yaliyokuwa yamevamiwa kwa kuanzishwa shughuli mbalimbali za kibinadamu hivyo ili kunusuru hilo serikali ikapanga kupanda miti ili kuongeza mapato ya serikali , kutoa ajira na kuongeza kipato kwa wananchi wanaozunguka hifadhi hiyo.

"Pia kutoa elimu kwa jamii zinazozunguka msitu huu juu ya uhifadhi na kutoa hamasa juu ya kilimo bora cha miti kwa kuzingatia matumizi ya mbegu bora," alisema Profesa Silayo.

Alisema, mashamba ya miti ni miongoni mwa misitu ya hifadhi za serikali kuu zinazosimamiwa na TFS ambayo yapo 23 nchini lengo likiwa ni kukidhi mahitaji ya mazao ya misitu.

Alisema TFS ina jukumu la kuendelea kuongeza mashamba mengine kwa ajili ya kuzalisha mazao mengi ya misitu kwani katika katika mwaka wa 2017/18 wakala uliongeza mashamba mapya manne.

Alitaja mashamba hayo kuwa ni Biharamulo lililopo Chato na Geita, Lyondo Msima lililopo Ileje na Songwe, Buhigwe (Kigoma) na Mpepo lililopo Mbinga Ruvuma.

Alisema shamba hilo ni miongoni mwa mashamba yaliyoanzishwa ili kuotesha na kukuza miti ya mbao laini na ngumu kwa ajili ya kutoa malighafi kwa viwanda vya misitu.

Vile vile kuhifadhi mazingira ya vyanzo vya maji, udongo na bioanuai zilizopotea, kulipatia taifa mapato ya misitu na huduma mbalimbali pamoja na kutoa ajira kwa wananchi.

"Uanzishwaji na uendelezaji wa shamba hilo unaenda sambamba na malengo ya serikali ya awamu ya tano ya kuwa na uchumi wa viwanda kwani malighafi itakapopatikana katika shamba katika hili baada ya miti kufikia umri wa kuvunwa itatumika katika viwanda vya kuzalisha karatasi, viwanda vya kuzalisha nguzo za umeme na vinginevyo," alisema.

Chanzo: www.habarileo.co.tz