Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania, Zambia zasaini hati nane za makubaliano

MoU Nane Zambia (600 X 374) Tanzania, Zambia zasaini hati nane za makubaliano

Thu, 26 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tanzania na Zambia zimesaini hati nane za makubaliano ya ushirikiano katika sekta mbalimbali ikiwemo sayansi, teknolojia na ubunifu, ulinzi, afya, gesi asilia, uwekezaji na biashara.

Makubaliano hayo yamesainiwa jana na kushuhudiwa na viongozi wa nchi zote mbili, Rais Hakainde Hichilema wa Zambia na Rais Samia Suluhu wa Tanzania ambao kwa pamoja wamesisitiza umuhimu wa makubaliano hayo kutekelezwa badala ya kutupwa kwenye makabati.

Kusainiwa kwa makubaliano hayo ni sehemu ya ziara ya kitaifa ya siku tatu ya Rais Samia Suluhu Hassan nchini Zambia ambayo imemalizika jana.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live