Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania, Zambia zaondoa vikwazo nane kati ya 24

Dkt Kijaji Awataka Wafanyabiashara Dodoma Kuchangamkia Fursa Tanzania, Zambia zaondoa vikwazo nane kati ya 24

Wed, 25 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tanzania na Zambia zimekubaliana kuendelea kuondoa vikwazo mbalimbali na kuweka mazingira wezeshi ya kufanyika kwa biashara na uwekezaji baina ya mataifa hayo yenye uhusiano wa karibu kihistoria.

Makubaliano hayo ni pamoja na kuondoa urasimu, kuweka mazingira rahisi ya ufanyaji biashara, kuitumia vyema miundombinu inayounganisha nchi hizo na kuruhusu muingiliano wa watu.

Hayo yamejadiliwa leo mjini Lusaka wakati wa kongamano lililowakutanisha wafanyabiashara wa Tanzania na Zambia na kwa pamoja wakakubaliana kuimarisha ushirikiano wa kibiashara baina ya mataifa hayo.

Akizungumzia hatua zinazoendelea kufanyika katika kuweka mazingira bora Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Ashatu Kijaji amesema tangu Agosti mwaka jana baada ya Rais Hichilema kutembelea Tanzania mawaziri wa kisekta wameshakutana mara kadhaa na wameondoa baadhi ya vikwazo visivyo vya kikodi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live