Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania, Zambia kumaliza changamoto za kibiashara

2006acfe 95db 4d23 8f2e De58547c6c2e.jpeg Tanzania, Zambia kumaliza changamoto za kibiashara

Fri, 14 Oct 2022 Chanzo: Eatv

Tanzania na Zambia zimedhamiria kumaliza changamoto za kibiashara na usafirishaji zinazowakabili wafanyabiashara ili kuruhusu biashara na usafirishaji wa bidhaa ufanyike bila vikwazo baina ya nchi.

Hayo yamebainishwa katika hotuba ya ufunguzi iliyosomwa na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine wakati wa Mkutano 10 wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano (JPC) kati ya Tanzania na Zambia ngazi ya Wataalam unaofanyika  jijini Lusaka Zambia.

Balozi Sokoine aliwasisitiza watendaji kutumia mkutano huo kuandaa mikakati ya pamoja itakayosaidia kuondoa vikwazo vya kibiashara na kutengeneza mazingira wezeshi kwa sekta ya umma na binafsi ili ziweze kufanya uwekezaji utakaoleta maendeleo endelevu kwa ajili ya maslahi mapana ya kiuchumi kwa pande zote mbili.

“Tanzania ina dhamira ya dhati ya kuimarisha ushirikiano wake wa kindugu na kihistoria na Zambia ili kuendeleza jitihada zilizoasisiwa na waasisi wa mataifa yetu kwa kuweka na mfumo rasmi wa ushirikiano unaowezesha ufuatiliaji wa utekelezaji katika masuala ya ushirikiano” alisema Balozi Sokoine.

Aidha, alieleza kuwa ushirikiano imara na wenye mafanikio ni ule unaojengwa kwa mfumo rasmi ambao unaruhusu kukutana na kufanya majadiliano ya mara kwa mara hivyo, alieleza kuwa ana amini kupitia mkutano huu maeneo yote ya ushirikiano yenye changamoto yatajadiliwa kwa kina kwa maslahi ya nchi zote mbili na wananchi wake.

Chanzo: Eatv