Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania, Uturuki mambo ni buli buli

Uturuki Tanzania Tanzaniaaa (600 X 342) Tanzania, Uturuki mambo ni buli buli

Thu, 7 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

TANZANIA itaendelea kushirikiana na Uturuki kuimarisha uhusiano uliopo kwa manufaa ya pande zote mbili.

Hayo yamesemwa jana Desemba 6, 2023 na Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk.

Balozi Mbarouk ameyasema hayo katika mazungumzo na Rais wa Taasisi ya Waturuki waishio Nje ya Uturuki na Jamii zao (YTB), Abdullah Eren katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Amesema, uhusiano kati ya Tanzania na Uturuki ni wa muda mrefu na unaoongoza hasa katika sekta za elimu, afya, biashara na uwekezaji na kuelezea matumaini yake kuwa uhusiano huo utaendelea kuimarika zaidi.

Naye Eren amesema, YTB ni Taasisi ya Uturuki inayojihusisha na utoaji fedha za ufadhili katika ngazi ya elimu ya juu kwa wanafunzi wa mataifa mengine na kusaidia juhudi za mtangamano za Diaspora wa Uturuki wanaoishi nje ya nchi hiyo.

Mazungumzo ya viongozi hao yamelenga kuimarisha uhusiano zaidi katika sekta ya elimu kati ya Tanzania na Uturuki na Mkutano huo umewezesha kubadilishana mawazo na uzoefu katika masuala mbalimbali yenye maslahi kwa pande mbili ikiwa ni pamoja na kuona jinsi ushirikishwaji wa diaspora unavyovyoweza kuchangia maendeleo ya kisiasa, kijamii na kiutamaduni katika nchi husika.

Katika tukio jingine, Balozi Mbarouk amekutana kwa mazungumzo na Balozi wa Saudi Arabia nchini, Yahya Ahmed Okesh na kujadiliana masuala mbalimbali ya ushirikiano baina ya mataifa yote mawili

Chanzo: www.tanzaniaweb.live