Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania, UAE zasaini ushirikiano utunzaji wa Mazingira

Thinjmkioo Tanzania, UAE zasaini ushirikiano utunzaji wa Mazingira

Tue, 7 Feb 2023 Chanzo: dar24.com

Taasisi ya Blue Carbon UAE na Serikali ya Tanzania kupitia Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) wametia saini Mkataba wa Makubaliano kuanza kwa ushirikiano wenye lengo la kukuza usimamizi endelevu wa misitu na kupunguza ukame.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Dkt. Selemani Jafo amesema biashara ya kaboni itasaidia kuleta fursa nyingi hapa nchini kuhifadhi mazingira katika hafla na Mwanamfalme wa Dubai ambaye pia ni Mwenyekiti wa kampuni ya Blue Carbon, Sheikh Ahmed Dalmook Al Maktoum na Waziri Maliasili na Utalii, Balozi Dkt. Pindi Chana.

Amesema, hii ni mara ya kwanza kwa makubaliano hayo baada ya Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kukamilisha uandaaji wa kanuni na mwongozo wa biashara ya kabini Oktoba 2022 na hatua hiyo itafungua milango kwa wananchi kupanda miti kwa wingi na kutunza mazingira, ili iweze kuingia kwenye biashara hiyo.

“Ni Imani yetu sasa tutategemea kuwa na fursa nyingi pamoja na kurudisha hali ya mazingira iliyoharibika na tunaona hata mikoko pia inaingia katika baishara ya kaboni hivyo TFS sasa watakuwa na uwanja mpana wa kuhakikisha misitu yetu inahifadhiwa,” amesema Jafo.

Kwa upande wake, Mwanamfalme, Sheikh Al Maktoum akiwa na ujumbe wake amesema ushirikiano huo utajikita katika kuunga mkono juhudi za Serikali za kuhifadhi, kusimamia na kusajili rasilimali zake za misitu.

Hifadhi hizo zenye ukubwa wa hekta milioni 8 katika awamu ya kwanza ya kwanza ikijumuisha hekta 56,000 za mikoko chini ya kifungu cha 6 cha Mkataba wa Paris hivyo kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizo mbili, katika kuendeleza miradi mipya ya kukabiliana na kaboni.

Chanzo: dar24.com