Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania, UAE mambo safi kwenye uwekezaji

Pesa Fedhaddd Tanzania, UAE mambo safi kwenye uwekezaji

Thu, 23 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali ya Tanzania imeuhakikishia Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) mazingira salama ya biashara na uwekezaji nchini.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk amebainisha hayo aliposhiriki katika kumbukizi ya miaka 52 ya Siku ya Taifa ya Umoja wa Falme za Kiarabu yaliyofanyika jana jioni Jijini Dar es Salaam na kuwasihi kuendelea kufanya biashara na kuwekeza kwa wingi nchini.

Balozi Mbarouk alisema kuwa, Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imefanya jitihada mbalimbali katika kuhakikisha kuwa mazingira ya biashara na uwekezaji yanaboreshwa ili kutoa fursa kwa wawekezaji wengi kuwekeza nchini.

Aliongeza kuwa Tanzania na Falme za Kiarabu zina ushirikiano mzuri wa kiuchumi katika eneo la biashara na uwekezaji ambapo UAE ni mshirika wa saba (7) wa kibiashara wa Tanzania kwa kiasi cha biashara baina ya nchi hizo kinachofikia Dola za Marekani bilioni 3.2. Kadhalika, kuhusu uwekezaji, UAE ni miongoni mwa nchi zilizowekeza kwa kiasi kikubwa nchini.

Balozi Mbarouk alipongeza juhudi za viongozi wa mataifa hayo, Tanzania Samia Suluhu Hassan na Rais wa UAE, Sheikh Mohamed bin Zayed Al Nahyan, kwa uongozi wao imara wenye maono na juhudi za kuimarisha na kudumisha uhusiano baina ya nchi hizi mbili .

Kwa upande wake, Balozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu nchini, Khalifa Abdulrahman Al Marzouqi alisema kuwa tangu kuanzishwa kwa uhusiano baina ya UAE na Tanzania mwaka 1974, nchi hizo zimejitahidi kuendeleza na kuimarisha uhusiano huo katika nyanja mbalimbali kwa maslahi ya pande zote mbili.

Aidha, Balozi Marzouqi aliishukuru Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano ambao imekuwa ikiutoa kwa UAE ambapo umesaidia kwa kiasi kikubwa kuboresha uhusiano baina ya mataifa hayo. -

Chanzo: www.tanzaniaweb.live