Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania Oman kufungua milango ya uwekezaji Nishati na Mafuta

OMANI Tanzania kurahisisha ufanyaji biashara na Oman.

Thu, 12 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tanzania na Omani zimedhamiria kukuza na kurahisisha mfumo wa kibiashara na uwekezaji katika sekta mbali mbali za kibiashara ikiwa ni pamoja nishati ya mafuta.

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amekutana Balozi wa Oman hapa nchini Balozi Ali Bin Abdallah Bin Salim Al Mahrouqi aliyemaliza muda wake wa uwakilishi hapa nchini ili kujadili suala hilo.

Rais Samia amekutana naye Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma na kumjulisha fursa mbali mbali za kibiashara.

Amemjulisha Balozi huyo kuwa kwa sasa Tanzania inapitia sheria na sera zake mbalimbali za biashara ili kujenga mazingira mazuri zaidi ya biashara na uwekezaji ikiwa ni pamoja na kuongeza ufanisi katika viwanja vya Ndege na Bandari ili kurahisisha ufanyaji biashara baina ya nchi hizi mbili.

Ikumbukwe kuwa Rais Samia alikutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa mambo ya nje wa Saudi Arabia Mwanamfalme Feisal Bin Farhan Al Saud Ikulu Jijini Dar es Salaam na kupeana fursa mbali mbali za biashara na uwekezaji baina ya mataifa hayo mawili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live