Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania, Kenya kuanzisha mfuko kulinda bonde la mto Mara

Mon, 16 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Serengeti. Tanzania na Kenya sasa zina mkakati wa kuanzisha mfuko wa kulinda Bonde la Mto Mara.

Akizungumza katika kongamano la wadau wa Mto huo kutoka Tanzania na Kenya lililofanyika leo Jumamosi Septemba 14,2019, Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Bonde la Ziwa Victoria kupitia Jumuiya ya Afrika Mashariki,  Dk Ali-Said Matano  amesema njia hiyo itasaidia kulinda mto huo muhimu kwa wananchi na viumbe hai.

Amesema kila nchi itawajibika kuweka fedha kwenye mfuko huo na wadau mbalimbali ili kuepuka hali ya kuomba fedha kila wanapotaka kufanya shughuli zao.

"Kupitia mfuko huo, kila changamoto inapojitokeza tutakuwa na uwezo wa kuitatua, kwa sasa Tanzania wameanza kuweka vigingi kutenga eneo la jamii na bonde la mto kwa Kenya hawajafanya, tukiwa na mfuko tutaweza kuweka maeneo yote ili kulinda bonde," amesema.

Dk Matano amesema maadhimisho ya nane ya Mara day mwaka 2019 yanakuja na mikakati mahsusi kupitia makubaliano yaliyosainiwa na nchi hizo ili kuwezesha utekelezaji wa makubaliano hayo kubwa ikiwa ni ulinzi wa ikolojia.

Pia Soma

Advertisement

Chanzo: mwananchi.co.tz