Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania, Cuba mambo ni 'buli buli'

Cuba Tanzania Tanzai (600 X 356) Tanzania, Cuba mambo ni 'buli buli'

Fri, 3 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango amekutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Cuba Salvado Valdés Mesa mazungumzo yao yaliofanyika katika Mji wa Baku nchini Azerbaijan.

Katika mazungumzo hayo Makamu Rais Dkt. Mpango amesema Tanzania na Cuba zimeendelea kuwa na uhusiano thabiti katika sekta mbalimbali za maendeleo kama vile Afya, Elimu, Viwanda na Biashara, pia ameishukuru nchi ya Cuba kwa kuendelea kushirikiana na Tanzania katika utoaji wa mafunzo hususani kwa kutoa ufadhili kwa Wanafunzi wa fani ya udaktari, michezo na fani nyinginezo pamoja na Wataalamu kutoka nchi hiyo kufanya kazi katika Hospitali mbalimbali nchini Tanzania.

Makamu wa Rais amesema Tanzania itaendeleza ushirikiano mzuri baina ya mataifa hayo mawili ulioasisiwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere na Rais Fidel Castro wa Cuba, uhusiano uliosaidia kwa kiasi kikubwa katika ukombozi wa nchi za kusini mwa Afrika wakati wa kupigani uhuru ambapo amesema kwa sasa uhusiano huo unaweza kuongezwa zaidi katika sekta za kilimo na utalii ambazo zitakuwa na manufaa kwa Mataifa yote mawili.

Kwa upande wake Makamu wa Rais wa Cuba, Salvado Valdés Mesa amesema uhusiano uliopo wa muda mrefu baina ya Tanzania na Cuba unathibitisha urafiki, umoja na ushirikiano wa kihistoria uliodumu katika Mataira hayo, pia ameishukuru Tanzania kwa kuendelea kuiunga mkono Cuba katika masuala mbalimbali katika jumuiya za kimataifa pamoja na nia yake ya dhati ya kuendelea kushirikiana na Cuba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live