Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania, China wajadili uchumi wa biashara

GHgNMSIWgAEw5Cc.jpeg Tanzania, China wajadili uchumi wa biashara

Thu, 29 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shule ya uongozi ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere iliyoko Kibaha, mkoani Pwani imekutanisha wawakilishi wa chama cha Kikomunisty cha nchini China (CPC) na wataalamu wabobezi kutoka vyuo vikuu kadhaa nchini kujadili maboresho ya mahusiano ya kimaendeleo kati ya Tanzania na China ili Tanzania inufaike kiuchumi na kupiga hatua za maendeleo kama ilivyo kwa China

Semina hiyo ya siku moja imefanyika kwenye shule ya uongozi ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambapo wataalamu hao wabobezi kutoka vyuo vikuu mbalimbali nchini wamekutana kujadili ya kufanyia maboresho katika sekta za Kilimo, uvuvi, utalii na ujenzi ili Tanzania na Afrika kwa ujumla iendelee kunufaika na uhusiano wa nchi ya China na chama cha CPC

Mkuu wa shule ya uongozi ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Prof. Macelina Chijoriga amesema yapo mambo kadhaa mazuri ya kujifunza Tanzania yakiwemo masuala ya ya uchumi na ya kijamii kutoka nchini China ili kujua namna China walivyofanikiwa kimaendeleo kuanzia miaka ya sitini hadi kufikia hatua iliyopo hivi sasa, ambapo inaelezwa awali mataifa hayo (Tanzania na China yalifanana kiuchumi

Mwakilishi wa CPC Jin Xin amesema China imekuwa na ushirikiano na nchi za Africa kwa kuimarisha mawasiliano na mahusiano na kwamba wanamengi ya kushirikiana na Tanzania na Afrika kwa ujumla wake katika sekta za kilimo, uvuvi, utalii na miundombinu

Amesema kujengwa kwa shule hiyo ya kwa ajili ya vyama sita (6) vya harakati za ukombozi wa nchi za Kusini mwa Africa ni moja ya mfano mzuri wa Tanzania na nchi ya China

Mmoja wa wabobezi hao waliokuwa katika majadiliano baina yao na wataalamu wa China kanali mstaafu George Simbakaria amesema jambo moja la kujifunza ni namna walivyotengeneza vizazi vyenye uadilifu na uadilifu kuanzia utotoni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live