Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania, China wajadili uchumi wa biashara

Majaliwa Waziri Naibu China Tanzania, China wajadili uchumi wa biashara

Wed, 24 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na Naibu Waziri Mkuu wa China Liu Guozhong na kugusia masuala kadhaa ya kiuchumi.

Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika leo Januari 23, 2024 mkoani Dar es Salaam, Viongozi hao pia wamezungumzia masuala ya biashara na uwekezaji ikiwemo ujenzi wa miundombinu kama vile viwanja vya ndege, barabara na uboreshaji wa nishati ya umeme.

Mazungumzo ya Waziri Mkuu Majaliwa pamoja Naibu Waziri Mkuu huyo wa China yamehudhuriwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko na viongozi wengine wa Serikali za Tanzania na China.

China inafanya uwekezaji katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo ujenzi wa miundombinu na imewekeza kwenye mradi wa Makaa ya mawe wa Liganga na Mchuchuma.

Naibu Waziri Mkuu wa China, Liu Guozhong yupo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live