Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania, China kubadilishana ujuzi kukuza utalii

China Tanznaia Utalii.png Tanzania, China kubadilishana ujuzi kukuza utalii

Thu, 8 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamisi Mwinjuma ‘Mwana FA’ amesema Serikali imeanzisha utaratibu wa makubaliano ya kubadilishana nyenzo na ujuzi kuitumia sekta ya utalii kati yake na China kuutangaza na kuukuza utamaduni.

Ametoa kauli hiyo jana Februari 7, 2024 alipokuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za kuadhimisha mwaka mpya wa China uliokusanya watu mbalimbali wa jamii hiyo nchini.

Akizungumza katika hafla hiyo iliyohudhuruliwa na mwenyeji wake Balozi wa China nchini Tanzania, Chen Mingjian, Waziri Mwinjuma amesema nchi hiyo ni moja ya mataifa wanayoshirikiana nayo katika sekta mbalimbali, hivyo watatumia fursa hiyo kukuza na kuutangaza utamadani.

“Mawazo yalikuwa ni kubadilishana ujuzi na uwezo wa kisanaa kati ya Tanzania na China katika kusherehekea mwaka mpya wa kichina na mchakato ulishaanza wa kukubaliana kubadilishana nyenzo na ujuzi katika eneo la utalii kukuza utamaduni wetu,” amesema Mwinjuma.

Mwinjuma ambaye ni Mbunge wa Muheza amesema kilichotokea katika sherehe hizo kwa kutumbuiza na kucheza nyimbo za kitamaduni za kichina na Tanzania ni mwanzo katika kutekeleza makubaliano waliyoaingia.

“Hata kaulimbiu yao ya mwaka wa kichina 2024 imejikita katika masuala ya utalii na utamaduni, nafikiri tutakuwa na mwaka mzuri wa dragoni za China utakaokuja kuonyesha mabadilishano mengi na utasaidia kuimarisha sekta zetu wote,” amesema.

Amesema ni mara yake ya kwanza kushiriki kwenye shughuli za Kichina, huku akieleza alikuwa akimwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan.

Awali, Balozi wa China nchini Tanzania, Mingjian amesema ni miaka 60 sasa mataifa hayo yana uhusiano wa karibu ulioasisi na marais wa nchi hizo na mategemeo yao wananchi watumia fursa hizo kujiinua kiuchumi.

“Mmejionea katika sherehe hizi ngoma za Kichina na Kitanzania zimechezwa ni katika kuendeleza na kudumisha uhusiano na tunataka fursa hizo zitumiwe na watu wetu kujijenga kiuchumi,” amesema Mngjian.

Amesema katika eneo la kidiplomasia tumefanikiwa kushirikiana kwa ukaribu na mafanikio makubwa, lakini shabaha yetu ni kuona hata maeneo mengine ikiwemo tamaduni zetu zinakua.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live