Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tantrade waongoza majadiliano tafiti hali ya biashara nchini

Pic Fedha Data Wastaafu Tantrade waongoza majadiliano tafiti hali ya biashara nchini

Mon, 11 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade), Latifa Khamis ameongoza zoezi la upokeaji na kuanza kwa majadiliano ya matokeo ya utafiti wa awali wa hali ya biashara nchini.

Taarifa iliyotolewa leo na Meneja Uhusiano kwa Umma na Masoko wa TanTrade, Lucy Mbogoro imeeleza kuwa zoezi hilo limefanyika leo Machi 11, 2024 katika Ukumbi wa Kilimanjaro kwenye Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.

Akizungumzia zoezi hilo, Latifa amesema utafiti huo wa hali ya biashara nchini uliofanyika mwaka 2023 ulihusisha mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Dodoma, Mbeya, Arusha na Unguja.

Amesema jumla ya kampuni 334 zilizosajiliwa na Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) pamoja na Wakala wa Usajili wa Biashara na Mali Zanzibar (BPRA) zilifanyiwa utafiti.

Latifa ametaja sekta zilizohusika wakati wa ukusanywaji wa takwimu kuwa ni kilimo, uvuvi, madini, utalii, viwanda, ujenzi, huduma ya fedha, bima pamoja na biashara za jumla na rejareja.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live